Ole Gunnar amewachana Liverpool kama klabu yenye ushindani mkubwa lakini ina ukame wa mataji! Anasema kitu kama hiki hakitakiwi Manchester United.
Manchester United wamekuwa washindani wakubwa katika miongo kadhaa na wakifanikiwa kupata ubingwa wa Ligi ya Uingereza mara 13 wakitawala ligi hiyo toka mwaka 1992 lakini wameshindwa kuinua taji hilo tena toka Alex Ferguson aliposepa.
Wakati wakielekea kuchuana leo Ole Gunnar amewatolea uvivu Liverpool ili watumike kama mfano kwa Man utd kutokuwa na kiu ya taji la ligi hiyo kwa mda mrefu. Liverpool wao kwa miaka 29 iliyopita wamekuwa washindaniaji tu lakini wanakosa nafasi ya kuibuka na ubingwa mara ya mwisho wakiwa wameshinda mwaka 1990.
Solskjaer anasisitiza kuwa Man Utd inatakiwa kurejea kileleni na kuwa watawala wa Ligi hiyo ili wasiwe tena wanatajwa kama wanaotaka kumaliza 4 bora tu. Bosi huyu wa msimu anasema anatambua kuwa ligi hiyo ni ngumu, pengine ni ngumu zaidi duniani lakini Manchester United wanatakiwa kukaza kamba kwenda sambamba na mbiuo za ligi hii.


Furahav
Ni kweli yuko sahii ole gunna