Chelsea wamekutana na City kwa awamu nyingine lakini ikiwa ni katika fainali ya kwanza kabisa ndani ya msimu huu na katika taifa hilo kuanza kushuhudiwa. Mchezo huo wa fainali ya Carabao ulishuhudia miamba hao wakimaliza dakika zao za kawaida bila kushuhudia nyavu kutikisika hadi kusukuma mechi hiyo kufika dakika 30 za ziada ili kumjua mbabe wa mechi hiyo.
Chelsea aliingia akikumbuka kubamizwa na City magoli 6-0 katika mechi zilizopita, amejitahidi kumzuia mbabe wake huyo na kumfanya ashindwe kabisa kupata hata goli la ushindi katika mtanange huo. Japo juhudi zao hazikuzaa matunda kutokana na kuipeleka mechi hiyo hadi hatua ya mikwaju ya penati ambazo ziliweza kuamua bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka huu.
Mstari mwekundu
Upande wa Chelsea, kuna hatari kubwa kwa kocha wao, kutokana na aina ya vipigo anavyovipokea, na kupoteza kwake mechi kunamfanya apoteze imani yake kwa matajiri wake juu ya uwezo wake kuendelea kukimudu na kukiendeleza kikosi hicho ambacho kwa sasa kina hatari kubwa kutokana na adhabu iliyotolewa na FIFA juu ya mipaka yake kufanya usajili.
Raia huyo wa Italia kwa sasa kibarua chake kipo katika mstari mwekundu kutokana na mwenendo wa matokeo ambapo wakati wowote kama matokeo yataonekana kuendelea hivyo hawezi kupata hata muda wa kuendelea kukikamatia kikosi hicho; endapo kikosi anachokifundisha hakina yale matokeo ambayo wamiliki wa klabu watayakubali matendo yake ndani ya kipindi hiki alichonacho.
Mtanange ulikaaje?
Hakuna ambacho kilionekana kuwazuia City ambao walikuwa kwenye kasi na ubora wa ajabu kuhakikisha wanaondoka na ushindi wa awali kabisa kuanza kuhesabu vikombe hivyo vinavyoingia ndani ya hifadhi zake baada ya msimu uliopita kuwa katika hali hiyo hiyo ambayo ilionekana kuwa na mvuto wa pekee baada ya City kushinda hatua ya matuta.
Makosa makubwa
Kilishuhudiwa kitendo kisichokuwa cha kiuungwana kabisa katika mechi hiyo ambapo mlinda mlango wa klabu hiyo Arrizabalaga aliweza kumfokea mwalimu wake akitaka kumlazimisha amtoe nje ya uwanja kwa alichodai yeye kuumia, jambo ambalo sio la kisoka kabisa kutokana na namna alivyomshambulia kocha huyo. Kitendo hicho kimekemewa na wakongwe wengi sana wa soka.
Mazingira hayo yalipelekea golikipa huyo kuonekana anafanya makusudi hata ilipokuja katika kuokoa mikwaju hiyo, ambapo alishindwa kabisa kutoa mpira uliopigwa na Aguero ambao ulionekana mwepesi sana kuokolewa na yeye.
Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Chris Sutton kwa maoni yake anaona kati ya Sarri na Kepa kama angepewa jukumu la nani aondoke: kwake yeye ilikuwa ni rahisi sana, angeshauri tu mlinda mlango huyo aondoke klabuni hapo na sio Sarri; maana anaonekana ni mwenye kukosa nidhamu na utu; kitu ambacho kwa kweli kimepelekea hata City wachukue ubingwa mbele yao.


Issa
Chelsea ilikuwa mnyera
Povel tz
Duh
Aziza mushi
Asanten kwa taarifaa.