Baada ya kutangazwa rasmi kama kocha wa muda wa Manchester United, sasa ni rasmi, Ralf Rangnick ataanza kazi ya kuiongoza United vs Crystal Palace.
Rangnick ametua United kwa mkataba wa kuiongoza timu hiyo kwa miezi 6 kama kocha wa mpito kisha, ataendelea kufanya kazi na United kama mshauri kwa miaka miwili.
Kutangazwa kwa Ralf Rangnick ilikuwa ni hatua ya kwanza, kuanza kazi rasmi ni hatua ya pili. Kufuatia taratibu za kufanya kazi nchini Uingereza, Rangnick alikuwa akisubiri kibali cha kumuwezesha kuanza kazi yake pale Old Trafford.
Mvumilivu hula mbivu, Rangnick amepatiwa kibali cha kufanya kazi na sasa ni rasmi, mchezo wake wa kwanza utakuwa dhidi ya Crystal Palace jumapili hii ndani ya Old Trafford.
Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.


