Joan Laporta ametuma ujumbe kwa Ousmane Dembélé huku kukiwa na kukwama kwa mazungumzo ya kandarasi.
Ousmane atamaliza mkataba wake na Barca msimu ujao wa joto, na jinsi mambo yalivyo, anaweza kuondoka klabuni hapo bure.
Barca wamedhamiria kukwepa suala la kuondoka bure, wana nia ya kumsainisha winga huyo kwa mkataba mpya mapema zaidi.
Lakini mazungumzo hayajaenda vizuri huku ripoti zikipendekeza kwamba, kwa jinsi mambo yalivyo, Dembélé ataondoka kweli msimu ujao wa joto.

Barca hawawezi kutoa mishahara ambao nyota huyu anahitaji anahitaji kwa sababu ya shida ya kifedha waliyonayo, lakini wakati huo huo, Laporta na mkufunzi mkuu Xavi Hernandez wanapendekeza Mfaransa kuwa ni sehemu muhimu ya mustakabali wa kilabu.
Laporta ametuma ujumbe kwa Dembélé wakati mazungumzo ya kandarasi yakiendelea kuzorota.
“Dembélé ni mchezaji muhimu sana, anaweza kutoa mengi zaidi kwa Barcelona kuliko alivyotoa. Ikiwa ataendelea na sisi, anaweza kufikia kuwa mchezaji wa kumbukumbu.”
Staa huyu amekuwa Barca tangu 2017 alipofikia kwa dili la thamani ya zaidi ya Euro milioni 130. Akiwa na miaka 24, bado kuna imani kwamba anaweza kufikia mafanikio makubwa akiwa Camp Nou.
Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.


