Nahodha wa Manchester United, Antonio Valencia ametoa ujumbe wake wenye hisia kali kwa mashabiki wake baada ya klabu kushindwa kuongeza kushinikiza ongezeko la mwaka mmoja kwenye mkataba wake klabuni hapo.
Bila shaka kwa wapenzi wa soka wanatambua nahodha huyu ambaye pia anacheza nafasi ya ulinzi klabuni hapo alivyokuwa mchezaji muadilifu na mwenye mapenzi ya kweli na klabu yake, alijitahidi kujitoa kadri alivyoweza kwa ajili ya Mashetani Wekundu kwa kipindi cha muongo mmoja alichokuwepo klabuni hapo.
Valencia aliingia United akitokea Athletic Wigan mwaka 2009, lakini wakati akiandamwa na majeraha kipindi hiki amekuwa hana bahati huku klabu hiyo iliyokuwa na uwezo wa kuongeza mwaka mmoja kwenye kufuatia makubaliano ya mkataba wake ambao unafika tamati ikishindwa kufanya hivyo kwa sababu ya ishu ya majeraha.
Nyota huyu katika ujumbe wake aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter anasema kuwa hakuwahi kufikiria kuwa angeweza kuondoka katika mji wa Lago Agrio wa Ecuador kwenda Ulaya lakini anamshukuru mungu kwa kumpa nafasi ya kwenda kucheza soka katika moja ya timu bora zaidi duniani kwa kipindi cha miaka 10. Anatarajia kupata ahueni ya majeraha yake kisha arejee kumalizia mda wake klabuni hao kwa kipindi kilichobakia kumaliza msimu.
Hata hivyo, kwa hali aliyonayo kwa sasa inaonekana kuwa kuna wasiwasi kama nyota huyu ataweza kurejea dimbani kabla ya msimu kuisha, na kama ikiwa hivyo basi anatarajiwa kuwa ataagwa vizuri zaidi klabuni hapo.


Warda
Jamani apone basi aongezewe mkataba #Meridianbettz
Furahav
Nenda tu mzee.
Caroline
Antonio yupo.vizuri
Povel
Bye bye 👋 legendary wetu tutakumic sana mzee wa kumwaga maji
Zeiyana
Kila la kheri mpambanaji Valencia