Ngoma Droo Spurs Wamshindwa Mgeni

Mauricio Pochettino aliingia dimnani leo dhidi ya Arsenal akiwa ameshapoteza matumaini kabisa ya kutwaa taji msimu huu. Kabla ya gemu ya leo alisisitiza kuwa Spurs wanahitaji muujiza labda ili waweze kutwaa taji hilo. Hata hivyo, gemu ngumu ya leo dhidi ya Arsenal imeenda ngoma droo! wamemaliza kwa sere ya 1-1!

Licha ya Spurs kumiliki mpira kwa asilimia 60 zaidi ya Arsenal waliomiliki asilimia 40 tu wameshindwa kubakiza pointi 3 nyumbani na kuwagawia wageni wao pointi moja.

Ngoma Droo Spurs Wamshindwa Mgeni
Penati imewasaidia Spurs kusawazisha

Arsenal wameanza kwa kuwashitua wenyeji wenyeji wao wakati Aaron Ramsey akicheka na nyavu dakika ya 16 tu. Gemu ikawa ngumu zaidi Tottenham wakishindwa kuona lango la wageni wao kipindi chote cha kwanza.

Madhambi ya Davinson Sanchez yaliwazawadia Spurs penati dakika ya 74 ambayo Harry Kane aliitumia vyema sana kusawazisha goli na kuwa mfungaji wa wakati wote kwenye debi za wawili hawa.

Spurs wamepiga jumla ya mashuti 10, na Arsenal pia wametandika mikwaju 9. Katika hiyo mikwaju iliyolenga goli ni mikwaju 3 tu kwa Spurs na 4 kwa Arsenal. Spurs wamekuwa na kona 3 wakati Arsenal wamekuwa nazo 4. Na faulo za Tottenham zilikuwa 15 wakati Arsenal zilikuwa 14.

Bila shaka ushindani unaendelea kuwa mkubwa zaidi huku Man United akitarajia kumpindua Arsenal mda sio mrefu ikiwa atamchapa Southampton.

2 Komentara

    Daah sikutegemea suluhu kwa spurs

    Jibu

    Spurs jeshiiiii

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.