Unampa Nani Umeneja wa Mwezi? Mameneja watatu wameingia kwenye kinyang’anyiro cha meneja bora wa mwezi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. Mameneja hawa ni Ole Gunnar Solskjaer wa Manchester United, Unai Emery na Pep Guardiola wa Manchester City.
Mshindi hapa anachaguliwa kwa muunganiko wa kura za mtandaoni zinazochangia asilimia 10 za kuamua nani mshindi na maamuzi ya paneli ya wataalamu wa soka.
Sir Alex Ferguson ndiye anayeongoza kwa kuchukua mataji ya meneja bora wa mwezi akiwa ameshinda mara 27. Guardiola pia anaingia kwenye 10 bora akiwa ameshinda mara 5. Ole Gunnar pia ameshinda tuzo mwezi uliopita ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa Man United toka alipoondoka Sir Alex Ferguson.
Tuwatazame kwa ufupi!
Unai Emery
Meneja huyu anaingia kwenye orodha hii wakati kikosi chake kilikuwa na mwanzo mbaya wa mwezi Februari wakianza kwa kupokea kichapo cha bao 3-1 dhidi ya Man City kabla gemu tatu mfululizo zilizofuata dhidi ya Huddersfield, Southampton, na Bournemouth. Wamerejea kwenye nafasi ambayo ilishikiliwa na Man Utd kwa mda. Hivye Emery ameshinda 3/4.
Ole Gunnar
United walikuwa na mwezi mgumu kidogo wakilazimika kucheza gemu 3 za ugeniuni na moja nyumbani kwa mwezi wa pili. Vijana wa Ole Gunnar walijitahidi kuhakikisha wanaenda sawa na hali ya Ligi wakifanikiwa kushinda gemu 3 dhidi ya Leicester City, Fulham na Crystal Palace na kutoa sare 1 dhidi ya Liverpool. Ole Gunnar ameshinda 3.5/4
Pep Guardiola
Kabla ya kuingia mwezi Februari walikuwa nyuma ya Liverpool. Mwezi Februari umewarudisha City mchezoni wakifanikiwa kuondoa gepu dhidi ya Liverpool. Man City wameshinda gemu zao zote dhidi ya Arsenal, Everton, Chelsea na West Ham. Wamefungwa goli 1 tu kwa gemu zote.
Ole Gunnar na Pep Guardiola ndiyo wanaonekana kuwa kwenye kinyang’anyiro kikubwa hapa! Unaweza kuwa na meneja wako wa mwezi weka kwenye kisanduku cha maoni
😀 📩


Povel
Pepe Hana faha kwl