Valencia Anasepa United, Ukepteni je

Klabu ya Manchester United wanaripotiwa kuwa wameamua kumchagua mchezaji mwingine atakayechukua nafasi ya Valencia kama nahodha wa klabu hiyo ikiwa nyota huyo atasepa klabuni hapo. Nani atauvaa ukepteni?

Taarifa zinadai kuwa nyota huyu anatarajiwa kusepa mwisho wa msimu huu baada ya kutumia miaka 10 klabuni hapo mkataba wake ukiwa unaisha msimu huu wa joto.

Valencia Anasepa United, Ukepteni je?
Pogba mbioni kuchukua majukumu ya Unahodha.

Taarifa pia zinataja kuwa nyota Paul Pogba yupo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuchukua nafasi hiyo kwa kipindi hiki. Kwa mujibu wa ripoti ya The Sun, Pogba ameonesha uwezo mkubwa wa uongozi kwa kipindi chote alichokuwa chini ya Ole Gunnar na anaaminika zaidi na meneja huyu tofauti na ilivyokuwa kipindi cha Mourinho.

Hata hivyo inasemekana mambo yanaweza kubadilika kama Bosi Ole Gunnar atafeli kupata kibarua cha kudumu klabuni hapo. Pogba anatarajia kuongeza idadi yake ya magoli 11 klabuni hapo pindi atakapoingia kukipiga dhidi ya Southampton.

Valencia Anasepa United, Ukepteni je
Valencia alikuwa mchezaji wa kwanza asiye muingereza kuichezea gemu 300 klabu ya Man United.
Kwanini Valencia anasepa?

Kwa mujibu wa ripoti jitihada za kufikia muafaka wa mazungumzo ya mkataba mpya wa nyota huyu zimegonga mwamba wakati staa huyu akiwa amebaikiwa na gemu kadhaa tu klabuni hapo hadi kumaliza msimu huu ambapo ndiyo mkataba wake unapooisha. Nyota huyu ataondoka kama mchezaji huru klabuni hapo.

2 Komentara

    Daah akiondoka litakuwa bonge la pengo.

    Jibu

    Valencia utakuwah pengo kubwa sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.