Donny van de Beek ameiomba klabu yake ya Manchester United kuweza kumuachia kuondoka kwenye klabu hiyo ili akapate nafasi ya kucheza mara kwa mara.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutokea Uholanzi amekuwa akikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara tokea akiwepo chini ya kocha alifungashiwa virago vyake Ole Gunnar Solskjaer, na sasa Ralf Rangnick ambaye naye hajavutiwa na huduma yake kwenye klabu hiyo.

Klabu ya Crystal Palace imevutiwa na huduma yake na wanaongoza kwenye mbio za kuhitaji saini yake, wakala wa van de Beek, Ali Dursun anafanya mazungumzo na klabu hiyo kuhusu uwezekano wa kuhamia kwa mkataba wa muda mfupi, ingawa Van de Beek bado anasubilia ikiwa klabu ya Man Utd watamruhusu kuondoka.
Van de Beek alinunuliwa kwa kiasi cha £35Milion kutoka klabu ya Ajax mwaka 2020, Tokea asajiriliwe ameichezea klabu ya Man Utd michezo 27 tu, huku akianza kwenye michezo miwili mwaka 2021 ya ligi kuu ya Uingereza.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.


