Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United na Leicester City Frank O’Farrell amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 94 kifo chake kimetangazwa leo siku ya jumatatu,
Frank O’Farrell aliongoza klabu ya Leicester City kwenye mchezo wa fainali ya FA Cup mwaka 169 na kupoteza kwa Manchester City, kwenye kipindi chake cha miaka mitatu alichotumia kwa mbweha hao

Frank O’Farrell alitambulika kama mrithi wa Matt Busby kama kocha wa manchester united mwaka 1971, ingawa alitumia miezi 18 baada ya hapo alifungashiwa virago mwezi december 1972 ambapo timu ya man utd ikiwa nafasi ya tatu kutoka chini na nafasi yake kuchukuliwa na Tommy Docherty.
Baadae aliifundisha Cardiff, timu ya taifa ya Iran na akaenda fundisha klabu ya falme za kiarabu Al-Shaab.
“kila mmoja wetu kwenye klabu ya manchester united amesikitishwa na kifo cha kocha wetu wa zamani Frank O’Farrell, man utd wakuandika kwenye mtandao wao.”
Pia klabu ya Leicester nao walitoa heshima yao kwa kocha wao wa zamani.
“Tumepokea kwa uchungu sana kusikia habari kwama kocha wetu wa zamani Frank O’Farrell ameaga dunia tarehe 6 machi 2022 akiwa na umri wa miaka 94.”
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


