Gamondi Ana Hasira na Ihefu

IKIWA yamesalia masaa machache, Yanga na Ihefu wacheze pale Azam Complex Chamazi, kocha wa Yanga Miguel Gamondi ameonesha wazi namna ambavyo alivyo na uhitaji wa alama tatu kwenye mchezo huo. Jisajili na Meridianbet upate bonasi kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

Ihefu vs Gamondi

Gamondi bado anakumbuka namna ambavyo alipoteza alama tatu mbele ya Ihefu kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza kwa mabao 2-1, jambo ambalo inaonekana ni wazi hatali lijirudie tena akiwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Gamondi anasema: “Binafsi sikufurahi kabisa tulivyocheza mchezo wetu dhidi ya Ihefu SC na kufungwa kwa mabao 2-1, najua pia hata mashabiki wetu hawakufurahi, nawakaribisha kesho kushuhudia burudani nzuri huku tukizipambania alama tatu muhimu.

Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.

“Najua haitakuwa mchezo rahisi kwetu, Ihefu wanaonekana wamebadilika na wamekuwa na matokeo mazuri kwenye mechi walizocheza hivi karibuni, kwahiyo nimewaambia wachezaji wangu wajue umuhimu uliopo kwenye huu mchezo na namna ambavyo tunahitaji kupata alama tatu,” amesema Miguel Gamondi.

Yanga wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara, kwa alama 46, wakiwa wamecheza mechi 17, wakisinda mechi 15, sare kwenye mchezo mmoja na kupoteza mechi moja, wamefunga mabao 49 na kuruhusu mabao tisa tu.

Wakati, Ihefu wao wapo kwenye nafasi ya 8, wakiwa na alama 23, wakicheza mechi 19, wameshinda mechi 6 tu, wakifungwa mechi mechi nane, sare kwenye mechi tano, wakiruhusu kufungwa mabao 23 na wao wakiwa wamefunga mabao 18. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Acha ujumbe