Kauli ya Kwanza ya Okrah Akiwa Yanga.

KIUNGO Mpya wa Yanga Augustine Okrah amesema kuwa klabu yake hiyo itakuwa ya moto sana kwenye eneo la ushambuliaji Kwa Sasa.

Okrah

Okrah ambaye awali alikuwa anacheza Simba kabla ya kurejea kwao Ghana Baada ya kushindwa kuwika Simba, alijiunga na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili na kucheza mechi yake ya kwanza Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi. Ukiwa na meridianbet odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.

“Natambua ubora wa kila mchezaji wa Yanga hususan maeneo ninayocheza, hilo linanifanya kuungana nao na kufanya vyema kwa ajili ya manufaa ya timu pia inanipa ari ya kupambana zaidi ili kupata nafasi kikosini.”

“Mimi sio mgeni hapa Tanzania, nimewahi kucheza Simba na sasa nimerudi nikiwa na Yanga nadhani tutakuwa na safu bora zaidi ya ushambuliaji na wapinzani wanapaswa kujipanga zaidi kutukabili.”

Okrah aliyewahi ichezea Simba Sc msimu uliopita kabla ya kuachwa na kurejea kwao katika timu ya Bechem United ambapo hadi anajiunga na Yanga alikuwa ameifungia mabao tisa (9) na kutoa pasi za mabao mawili (2) katika mechi 16.

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi akimzunguzia Okrah, alisema ni mchezaji mzuri na kama atafanya vyema mazoezini basi atampa nafasi.

“Nimemuona ni mchezaji mzuri, kama ilivyo kawaida, natoa nafasi kwa mchezaji anayefanya vizuri mazoezini kwani tunachokifanya kwenye uwanja wa mazoezi ndicho tunafanya kwenye mechi, hivyo kila mtu ndani ya timu yetu ana nafasi kikosini,” alisema Gamondi.

Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Acha ujumbe