OKRAH ATOA KAULI YA KIBABE

KIUNGO raia wa Ghana Augustine Okrah amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu kwani amekuja kufanya kazi na kuonesha kipaji Chake.

Okrah alitambulishwa juzi visiwani Zanzibar na anatarajia kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu hiyo Baada ya kuanza mazoezi pamoja na timu.OKRAH“Kabla ya kusajiliwa na Yanga tulikaa kuzungumza na Raisi Eng Hersi. Ambapo tulizungumza mambo mengi zaidi ambayo yalisababisha niweze kukubali kujiunga na Yanga.

“Malengo ya timu kwa ujumla na jisni ambavyo alikuwa akinipa mipango yake, ya timu na jinsi gani natakiwa kujiunga na Yanga yalinishawishi kukubali.

“Mipango ya timu kuhakikisha kuwa kimataifa msimu huu inafika katika hatua ya robo fainali ni jambo ambalo aliniambia kuwa natakiwa kuwa sehemu ya mchango huo kwa kuwa anaamini katika uwezo wangu,hivyo kilichobaki ni kwangu kuwaonyesha wanayanga kazi ambayo imenifanya nije.OKRAH“Na ninaomba waamini na kujua kuwa nimekuja kufanya kazi na kuonesha kipaji changu na nitafanya hivyo Kwa hakika,” alisema Okrah.

Acha ujumbe