Sancho Kurejea Dortmund

Winga wa klabu ya Manchester United Jadon Sancho inaelezwa anaweza kutimkia klabu yake ya zamani Borussia Dortmund baada ya kushindwana na kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag.

Klabu ya Borussia Dortmund inaelezwa kufanya mazungumzo na klabu ya Manchester United juu ya kupata huduma ya Sancho kwa mara nyingine tena, Kwani hata mchezaji huyo ameonesha nia ya kutaka kutimka klabuni hapo.sanchoWinga huyo raia wa kimataifa wa Uingereza aliingia kwenye mzozo na kocha wa klabu yake Erik Ten Hag mapema mwezi Septemba mwaka jana, Kupitia sakata hilo limepeleka mchezaji huyo kutocheza ndani ya klabu hiyo mpaka leo.

Manchester United wanaelezwa kua tayari kuchukua ofa ya mchezaji huyo kutoka timu yeyote itakayomuhitaji, Lakini taarifa zinaeleza kua Borussia wanafikiria kumsajili mchezaji huyo kwa mkopo wa nusu msimu.sanchoMchezaji Jadon Sancho mpango wake ni mmoja tu kutimka ndani ya viunga vya Old Trafford, Kwani alishindwa kuomba radhi kwa kocha wake Erik Ten Hag hivo milango imefunguliwa kwa yeye kutimka ndani ya timu hiyo na Dortmund ndio wanaongoza mbio mpaka sasa.

Acha ujumbe