Winga wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uingereza Jadon Sancho inaelezwa ameshikilia msimamo wake wa kutotaka kuomba msamaha kwa kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag.

Sancho alipishana na kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag baada ya kocha huyo kusema mchezaji huyo hakuonesha kiwango kizuri mazoezini kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Arsenal, Huku ikiwa sababu ya mchezaji huyo kutokucheza mchezo huo.sanchoMchezaji huyo alikuja na andiko ambalo alilichapisha katika mtandao wake wa kijamii wa X zamani (Twitter) akieleza kua kocha huyo amemtumia kama kichaka cha kujifichia baada ya kupoteza mchezo huo dhidi ya klabu ya Arsenal.

Baada ya kupishana na kocha wake mchezaji huyo alipewa sharti moja la kuomba radhi kwa kocha huyo mbele ya wachezaji wenzake, Lakini winga huyo amegoma kuomba radhi mpaka leo licha ya kuelezwa na baadhi ya viongozi klabuni hapo na hata baadhi ya wachezaji wenzake.sanchoBaada ya kuelezwa kua Jadon Sancho hana mpango wa kuomba msahama kwa kocha Erik Ten Hag ili arudi ndani ya timu hiyo, Ni wazi mchezaji huyo yuko mbioni kuachana na klabu ya Manchester United katika dirisha dogo la mwezi Januari.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa