Kiungo wa klabu ya Manchester City Matheus Nunes ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ureno baada ya kuelezwa kupata majeraha ya misuli akiwa na timu hiyo.

Matheus Nunes amefanyiwa vipimo katika kambi ya timu ya taifa ya Ureno na kubainika kua hataweza kucheza katika michezo miwili ya timu ya taifa ya Ureno kati ya Liechtentien pamoja na Iceland.nunesMchezaji huyo bado haijafahamika ataweza kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha muda gani kutokana na majeraha ya misuli ambayo imekua ikimuandama na kumfanya kuondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa.

Kiungo Matheus Nunes ambaye amejiunga na klabu ya Manchester City katika dirisha kubwa msimu huu, Bado hajafanikiwa kuonesha cheche ambazo alikua akionesha katika klabu ya Wolverhampton.

 JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa