Kocha wa zamani wa vilabu vya Sevilla na Wolverhampton Julen Lopetegui inaelezwa ameipiga chini ofa ya klabu inayoshiriki ligi kuu ya Saudia Arabia Al Ittihad baada ya kumfukuza kocha wake.
Klabu ya Al Ittihad imemfukuza aliyekua kocha wake Nuno Espirito Santo siku kadhaa nyuma ilifanya jitihada za kumpata kocha Julen Lopetegui, Lakini kocha huyo ameipiga chini ofa hiyo.Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Wolves aliachana na Wolves mwishoni mwa msimu huu uliomalizika baada ya kushindwana katika baadhi ya vipengele, Hivo kumfanya kocha huyo kutokua na kibarua mpaka wakati huu.
Kocha Julen Lopetegui inaelezwa chanzo cha kukataa ofa ya klabu ya Al Ittihad ni kwasababu ana mipango ya kutafuta timu ambayo inashiriki ligi kuu ya Uingereza japo bado bado hajaipata.Klabu ya Al Ittihad inaelezwa baada ya kocha huyo wa kimataifa ya Hispania klabu hiyo ipo kwenye hatua za mwishoni na kocha raia wa kimataifa wa Argentina Marcelo Gallardo.