Kocha wa klabu ya Everton Frank Lampard anatumai kukutumia kikosi kilekile alichokitumia kwenye mchezo dhidi ya Chelsea jumapili iliyopita kwenye mchezo ambao alishinda kwa 1-0 kwenye safari yake ya kwenda kuwavaa Leicester city kwenye dimba la King Power wikiendi hii.

Lampard anasema baaada ya mchezo dhidi ya Chelsea kuisha kulikuwa na sintofahamu kidogo kutoka kwenye timu yake, ambapo Richarlison bado hayuko sawa kutokana na kupata majera kidogo ambayo aliyapata kwenye mchezo dhidi ya Liverpool, japo alifanikiwa kucheza kwenye mchezo dhidi ya Chelsea na kufunga goli la ushindi.

Lampard
Frank Lampard

“Richarlison alipata majeraha kidogo ya ankle tulipocheza na liverpool, lakini natumai atakuwa sawa,” alisema Lampard kwenye kikao na waandishi wa habari kabla ya mchezo wake wa wikiendi hii.

Kocha huyo pia alithibitisha kutokuwepo kwa Ben Godfrey na Donny van de Beek, ila André Gomes yuko sawa kuwakabili Leicester baada ya kuwa nje kwa muda kidogo akisumbuliwa na tissue.

“Ben hayuko sawa ila tunatumai atarudi katikati ya wiki inayokuja na kuanza mazoezi”, Lampard aliongezea baada ya mchezaji huyo kutolewa kwenye mchezo dhidi ya liverpool


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa