Mei 8 kila mwaka, huwa ni siku maalumu ya kusherehekea maisha ya kinamama kote duniani. Hawa ni watu muhimu kwenye uzazi, malezi, ustawi na maendeleo ya jamii zetu. Neno mama ni neno fupi lakini, lina maana kubwa kwenye maisha ya mwanadamu. Kwa kutambua umuhimu wa kinamama, Meridianbet iliamua kusheherekea pamoja nao.

Ni desturi ya Meridianbet kurejesha kwa jamii na safari hii, siku maalumu ya kusherehekea kinamama ilinogeshwa zaidi na kapu la bi mkubwa kutoka Meridianbet. Kama wanavyotambulika kwa kuwa mabingwa wa Odds na Bonasi kubwa kwenye michezo ya kubashiri, vivyo hivyo Meridianbet imewatambua na kuwaongezea tabasamu kinamama wanaojishughulisha na kazi mbalimbali za kujipatia kipato.

Wapo wasusi, wavuvi, washonaji nguo, wauza mbogamboga, wauza vyakula almaarufu ‘mama ntilie’ na wafanyabiashara wengine wengi wadogo wadogo. Wote hawa ni sehemu ndogo ya kinamama wengi nchini wanaowekeza nguvu na muda wao katika kazi ya kujipatia kipato ili kukidhi mahitaji yao na familia zao.

Meridianbet, Meridianbet Yatoa Kapu La Sikukuu Ya Kinamama, Meridianbet
Mabalozi wa Meridianbet, Jacob Mbuya (fulana nyeupe) na Foby (katikati) wakifurahi na kina mama wajasiriamali wa Manzese, Dar es Salaam.

Kwa kutambua mchango na juhudi zao, Meridianbet ilifanya ziara fupi katika masoko ya Tandale, Manzese na Msasani jijini Dar es Salaam na kuwapongeza baadhi ya kina mama wanaofanya shughuli zao ndogo ndogo kwenye maeneo hayo.

Akizungumza na Meridianbet baada ya kupokea zawadi kutoka kwenye kampuni hiyo, mmoja ya kina mama hao (hakutaka jina lake kuwekwa hadharani), ameishukuru kampuni hiyo kwa kuungana nao na kuwaongezea thamani kwenye majukumu yao. Pamoja na hayo, ameiomba kampuni hiyo kuendelea kuifikia zaidi jamii na pia kuwawezesha kinamama kwa kuwaongezea kwenye mitaji yao midogo ili waweze kuzikuza biashara zao wanazozifanya.

Meridianbet, Meridianbet Yatoa Kapu La Sikukuu Ya Kinamama, Meridianbet
Balozi wa Meridianbet, Foby akikabidhi zawadi kwa mama mjasiriamali katika soko la Tandale, Dar es Salaam

Kwa upande wa kampuni hii, Afisa Mahusiano ya Jamii, Ndugu. Amani Maeda, amewapongeza kinamama wote nchini kwa kazi kubwa wanayoifanya hasa katika malezi ya jamii na, ameendelea kuwatia moyo kina mama wote wanaojishughulisha na kazi ndogondogo za kijikwamua kiuchumi. Bwana Maeda aliongezea kuwa, kampuni hiyo itaendelea kuwa karibu na jamii na itaendelea kuwafikia zaidi kwa kadiri itakavyowezekana.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

 

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa