Mshambuliaji nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, ametangaza rasmi kuwa ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, akihitimisha safari yake ya mafanikio iliyodumu kwa miaka tisa tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2017 akitokea AS Roma.
Kupitia taarifa aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii, Salah amesema uamuzi huo haukuwa rahisi, akisisitiza jinsi klabu hiyo, jiji la Liverpool pamoja na mashabiki wake walivyokuwa sehemu muhimu ya maisha yake. “Kwa bahati mbaya, siku hii imefika. Hii ni sehemu ya kwanza ya kuaga kwangu. Nitaondoka Liverpool mwishoni mwa msimu,” amesema nyota huyo wa Misri.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika kipindi chake cha mafanikio ndani ya Liverpool, Salah amefunga mabao 255 katika mechi 453, na kuwa mfungaji wa tatu kwa ubora katika historia ya klabu hiyo. Akiwa Anfield, alichangia timu kushinda mataji makubwa ikiwemo Ligi Kuu England, Ligi ya Mabingwa Ulaya, FA Cup, Kombe la Ligi pamoja na Kombe la Dunia la Klabu.
Salah ameongeza kuwa mafanikio hayo yalikuja sambamba na changamoto, lakini mshikamano alioupata kutoka kwa mashabiki ulimpa nguvu ya kuendelea. “Hatukushinda tu mataji makubwa, bali pia tulipambana pamoja katika nyakati ngumu zaidi za maisha yangu. Sitoweza kusahau sapoti yenu,” alieleza.
Msimu huu, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 amekuwa na kiwango cha wastani chini ya kocha mpya Arne Slot, akifunga mabao matano na kutoa pasi sita za mabao katika mechi 22 za Ligi Kuu, huku Liverpool ikipambana kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Kwa upande wake, klabu ya Liverpool imeelezea mchango wa Salah kuwa wa kipekee na wa kukumbukwa, ikibainisha kuwa taarifa hiyo imetolewa mapema ili kutoa uwazi kwa mashabiki.
“Kuondoka si jambo rahisi, lakini nitabaki kuwa mmoja wenu milele. Klabu hii itabaki kuwa nyumbani kwangu na familia yangu. Asanteni kwa kila kitu, kwa sababu yenu sitatembea peke yangu,” alihitimisha Salah.

