Felix Zwayer Apewa Mechi ya  Kombe la Dunia Licha ya Historia ya Upangaji Matokeo

Mwamuzi wa Ujerumani, Felix Zwayer, ambaye aliwahi kutiwa hatiani kwa tuhuma za upangaji matokeo mwaka 2005, ameteuliwa kuamua mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia kati ya Denmark na North Macedonia utakaopigwa Alhamisi usiku katika Uwanja wa Parken.

Felix Zwayer Apewa Mechi ya  Kombe la Dunia Licha ya Historia ya Upangaji MatokeoZwayer mwenye umri wa miaka 43 aliwahi kufungiwa kwa miezi sita na German Football Association mwaka 2005 kufuatia kuhusika kwake katika kashfa ya upangaji matokeo. Adhabu hiyo ilitokana na kazi yake kama mwamuzi msaidizi chini ya Robert Hoyzer, ambaye alikutwa na hatia ya kupokea rushwa ili kupanga matokeo ya michezo kadhaa ya Ligi Daraja la Pili nchini Ujerumani.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Kwa mujibu wa taarifa, Zwayer alidaiwa kupokea euro 300 kabla ya mchezo ulioshirikisha timu ya Wuppertaler SV, hata hivyo baadaye alichukua hatua ya kuripoti vitendo hivyo kwa shirikisho la soka la Ujerumani, akisaidiwa na waamuzi wengine watatu waliothibitisha madai yake dhidi ya Hoyzer.

Felix Zwayer Apewa Mechi ya  Kombe la Dunia Licha ya Historia ya Upangaji MatokeoKashfa hiyo haikujulikana kwa umma hadi mwaka 2014 baada ya gazeti la Ujerumani Die Zeit kuchapisha uchunguzi maalum ulioitwa “The Zwayer File”, ulioweka wazi historia ya adhabu hiyo. Wakati huo huo, Hoyzer alifungiwa maisha yote kujihusisha na soka.

Mwaka 2021, kurejea kwa Zwayer katika uamuzi wa mechi kubwa kulizua mjadala, ambapo kiungo wa Borussia Dortmund, Jude Bellingham, alimkosoa wazi baada ya mchezo dhidi ya Bayern Munich akisema: “Unampa mwamuzi aliyewahi kupanga matokeo mechi kubwa zaidi nchini Ujerumani, unatarajia nini?”

Felix Zwayer Apewa Mechi ya  Kombe la Dunia Licha ya Historia ya Upangaji MatokeoHata hivyo, Zwayer anaendelea kuaminiwa na mamlaka za soka, ambapo ni siku tano tu zimepita tangu aliposimamia mchezo mwingine muhimu nchini Denmark kati ya FC Midtjylland na Nottingham Forest katika michuano ya Europa League.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.