Crystal Palace Yamnyatia Andoni Iraola Kuchukua Nafasi ya Oliver Glasner

Klabu ya Crystal Palace inaripotiwa kupanga kufanya jaribio la kumsajili kocha wa AFC Bournemouth, Andoni Iraola, katika dirisha la majira ya kiangazi huku ikijiandaa kuachana na kocha wake wa sasa Oliver Glasner mwishoni mwa msimu huu.

Crystal Palace Yamnyatia Andoni Iraola Kuchukua Nafasi ya Oliver GlasnerTaarifa zinaeleza kuwa Palace imeingia kwenye mbio za kumwania Iraola kufuatia pia kuibuka kwa nia kutoka kwa Athletic Club, hali inayoongeza uwezekano wa kocha huyo kuondoka Bournemouth pindi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Iraola alizungumzia tetesi hizo baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Manchester United, akisisitiza kuwa bado ana furaha kuendelea kubaki katika klabu yake ya sasa. “Hapana, hilo halihusiani na mimi. Labda kama shabiki kwa sababu ni klabu yangu, lakini haliathiri chochote,” alisema.

Crystal Palace Yamnyatia Andoni Iraola Kuchukua Nafasi ya Oliver GlasnerKocha huyo aliendelea kueleza kuwa ana uhusiano mzuri na klabu na suala la mustakabali wake si jambo jipya kwake. “Nimesema mara nyingi, nina furaha hapa. Nina mahusiano mazuri na klabu. Ni kweli tutalazimika kufanya maamuzi kulingana na hali ilivyo, lakini si jambo jipya kwangu kama kocha,” aliongeza Iraola.

Kwa mujibu wa taarifa, Palace inafikiria kutoa ofa ya kushtua ambayo inaweza kusababisha uhamisho wa nadra kati ya klabu mbili za Ligi Kuu England, ikiwa watafanikiwa kumshawishi Iraola kuhamia kusini mwa London.

Crystal Palace Yamnyatia Andoni Iraola Kuchukua Nafasi ya Oliver GlasnerTangu ajiunge na Bournemouth, Iraola ameshinda mechi 37 kati ya 107 za ligi nchini England ndani ya takribani miaka mitatu, huku timu yake ikiwa imefunga mabao 158 na kuruhusu 161.

Kwa sasa Bournemouth ipo juu ya Palace kwenye msimamo, ikiwania nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya huku klabu mbalimbali zikizidi kuonyesha nia ya kumtaka kocha huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.