Romelu Lukaku Ajitoa Kikosi cha Timu ya Taifa ya Ubelgiji

Mshambuliaji nyota wa Ubelgiji, Romelu Lukaku, amejiondoa katika kikosi cha timu ya taifa kitakachosafiri kuelekea Marekani kwa ajili ya michezo ya kirafiki ya kujiandaa na Kombe la Dunia, itakayofanyika katika miji ya Atlanta na Chicago.

 Romelu Lukaku Ajitoa Kikosi cha Timu ya Taifa ya UbelgijiLukaku mwenye umri wa miaka 32, ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Ubelgiji akiwa na mabao 89 katika mechi 124 za kimataifa, ameamua kujikita zaidi katika kuboresha hali yake ya mwili badala ya kushiriki michezo hiyo dhidi ya Marekani na Mexico.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Kupitia taarifa rasmi, ya Shirikisho la Mpila wa miguu Ubelgiji ilieleza sababu ya uamuzi huo ikisema: “Romelu amechagua kujikita katika mazoezi ili kuboresha zaidi utimamu wake wa mwili.”

 Romelu Lukaku Ajitoa Kikosi cha Timu ya Taifa ya UbelgijiMsimu huu, Lukaku amekuwa akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara yaliyomfanya kucheza mechi chache katika klabu yake ya SSC Napoli, hali iliyochangia uamuzi wake wa kujiondoa katika ratiba ya timu ya taifa.

Mara ya mwisho kwa Lukaku kuichezea Ubelgiji ilikuwa mwezi Juni katika ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Wales national football team kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia uliopigwa Brussels, ambapo pia alifanikiwa kufunga bao.

 Romelu Lukaku Ajitoa Kikosi cha Timu ya Taifa ya UbelgijiBaada ya mchezo huo, mshambuliaji huyo alikosa michezo sita iliyofuata ya kimataifa, huku sasa akilenga kurejea katika kiwango chake bora kabla ya michuano mikubwa ijayo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.