Psg Kuwaalika Juventus

Michuano ya ligi ya mabingwa kuanza hii leo ambapo kundi H litawakutanisha miamba wa Ufaransa Paris Saint German (PSG) dhidi ya Juventus kutoka Italy huku Psg ikiwa na wachezaji wenye vipaji vikubwa pale Ligue 1.

 

Psg Kuwaalika Juventus

Psg ikiwa na wachezaji kama vile Lionel Messi, Mbappe, Neyma, na wengine wengi wataanzia nyumbani kutafuta alama tatu ambazo zitakuwa na umuhimu kwao halikadhalika kwa Juventus ambao watakuwa ugenini watahitaji kupata ushindi katika mechi hiyo.

Timu hiyo ambayo ipo chini ya kocha wake Christophe Galtier msimu uliopita iliishia katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambapo aliondolewa na mabingwa  watetezi wa kombe hilo Real Madrid baada ya kutofunga mabao mengi ambaye yangeweza asonge mbele katika hatua ya nusu fainali.

Psg Kuwaalika Juventus

 

Kwa kushindwa kwa Psg kusonga mbele kwenye michuano hiyo wakaamua kumfukuza kocha wao wa kipindi hicho Mauricio Pochettino na kumleta kocha mpya kuja kukinoa kikosi hicho kilichojaa wachezaji ambao wana uwezo mkubwa. Wakati kwa upande wa Juventus wao walitolewa kwenye hatua ya makundi na Chelsea.

 

Psg Kuwaalika Juventus

Psg kwenye Ligue 1 amecheza michezo sita ameshinda mitano, sare moja na hajapoteza mchezo mmoja akiwa kileleni katika ligue 1,. Wakati kwa upande wa Juventus katika Serie A ndani ya michezo mitano ameshinda michezo miwili, sare tatu, akiwa hajapoteza pia na kwenye msimamo yupo nafasi ya saba.

 

Acha ujumbe