PSG Wabakia Kileleni Ligue 1.

PSG mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 wameendelea kubaki kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Paris saint German walifanikiwa kupata ushindi wa goli tatu kwa bila dhidi ya klabu ya Nantes magoli mawili ya Klian Mbappe na beki raia wa kireno Nuno Mendes aliefunga goli moja ilitosha kuwafanya klabu hiyo kubaki kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu Ufaransa.

psgParis wanaongoza ligi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa kwani wamelingana alama na klabu ya Olympique Marseille ambao wana alama 16 sawa na PSG baada ya kucheza michezo sita na kushinda mitano huku wakisuluhu mchezo mmoja.

Kwenye mchezo mjadala bado unaendelea kwa mchezaji wa klabu hiyo Lionel Messi ambayee anaonekana kuendelea kuonesha kiwango kizuri licha ya umri wake kuonekana umesogea baada ya jana kupiga pasi mbili zilizozaa mabao kwenye mchezo huo na mabao hayo yote yalifungwa na Klian Mbappe.

Acha ujumbe