Willian Mbioni Kwenda Fulham.

Huku tetesi zikizidi kuendelea Willian Borges ambaye alikuwa ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na Arsenal akaribia kujiunga na Fulham ambao wamepanda ligi msimu huu baada ya kushuka daraja msimu uliopita.

Willian Mbioni Kwenda Fulham.

Willian mwenye umri wa miaka 34 alipata mafanikio makubwa akiwa na Chelsea na baadae baada ya kushindwana kwenye kipengele cha mkataba aliamua kutimkia kwa The Gunners mwaka 2020 ambapo alikuwa sio chaguo la kwanza la mwalimu Mikel Arteta, Hivyo kujikuta akikaa benchi kwa muda mrefu bila kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Kutokana na kukaa benchi kwa muda William aliamua kurudi nyumbani kwao Brazil msimu uliopita na kwenda kujiunga na timu ya Corianthias ambayo makao makuu yake yapo Sao Paulo nchini Brazil.

Willian Mbioni Kwenda Fulham.

Willian na wawakilishi wapo kwenye uwanja wa mazoezi wa Fulham na Mbrazil huyo yupo mbioni kutia saini mkataba kwenye klabu hiyo kwani amekuwa akifanya mazoezi kwa muda wa wiki mbili zilizopita na kikosi cha kwanza cha Fulham baada ya kuvunja mkataba wake na Corinthians. Kocha wa timu hiyo amekuwa akivutuwa na Willian kutokana na kile anachokionesha mazoezini na kumuona kama ni mtu ambaye anaweza kuongeza ubora kwenye kikosi chake.

Acha ujumbe