Mshambuliaji wa Manchester City, Kun Aguero amejiunga na Barcelona kama mchezaji huru na yupo tayari kusaini katika majira ya kiangazi.
Agüero amefikia makubaliano ya maneno kwaajili ya kusaini kandarasi hadi 2023 na mshahara wa € 10m.
Anatarajiwa kusaini kandarasi yake na Barça baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa, kuna ziada pia iliyojumuishwa ikiwa Barcelona itashinda Ligi ya Mabingwa katika miaka miwili ijayo.
Barcelona pia wanakaribia kumsajili Memphis Depay kama mchezaji huru. Amewathibitishia mawakili wake wapya kwamba anataka kujiunga na Barça – mazungumzo yanaendelea.
Agüero atajiunga hivi karibuni, alikubali pendekezo hilo. Na kama @verobrunati alivyoripoti pia ana ndoto ya kucheza na Leo Messi.
Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.