Ahmed Ally: Hakuna Njia Ahly Kuepuka Kipigo cha Simba SC

UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi kuwa mpango mkubwa kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ni kupata ushindi Kwa nguvu ya namna yoyote ile. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Simba

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema hesabu kubwa ni kupata matokeo chanya kwenye mchezo huo na ndiyo maana wakachagua kwenda Zanzibar kujifua.

“Hapa ni kupata ushindi tu dhidi ya Waarabu wa Misri huku mtego mkubwa ikiwa ni kubadilika kulingana na namna wapinzani watakavyokuja katika mchezo husika.

“Kwa namna yoyote Al Ahly Lazima apasuke Kwa Mkapa na hiyo ndiyo dhamira yetu tuliyonayo. Tuna Imani na timu yetu na tunajua ubora wa kikosi chetu na Lazima tushinde.”

Aliongeza pia mechi hiyo wataimalizia nyumbani kwa Mkapa kisha wakienda Misri ni mwendo wa kushikilia bomba tu mpaka mwisho wa mchezo.Β  Jisajili na Meridianbet upate bonasi za kasino kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

“Benchikha ni miongoni mwa silaha zetu muhimu kuelekea mchezo wetu wa Machi 29, 2024 [Simba V/s Al Ahly, Benchikha ni kocha mkubwa mwenye wasifu mkubwa ambaye anaweza kucheza mechi kama hizi.

“Ndio maana nasema, kwetu mechi hii ni ya mkondo mmoja tu! Tutahangaika kuhakikisha tunaimaliza hii mechi Dar es Salaam”.

“Uwezo wa kushikilia bomba β€˜kuzuia/kujilinda’ Simba tunao, tuliona hapa dhidi ya Wydad tulishinda 2-0 tukashikilia bomba mpaka mechi ikaisha”.

“Kule nyumbani kwao [Wydad] tulishikilia bomba mpaka dakika ya 93, makosa madogo yakapelekea tukaadhibiwa. Simba hatuwezi kuzuiliwa na Al Ahly, wanasimba tumeamua jambo letu, Al Ahly anafia Benjamin Mkapa”.

Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.

Acha ujumbe