Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amewataka wachezaji wake kuonyesha kiwango cha juu kwenye mchezo watakapokutana na Bayer Leverkusen katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku timu hizo zikiwa zimefungana 1-1 kwenye mchezo wa kwanza.
Arteta alisema kuna mambo mengi yatakayochangia mafanikio ya timu yake kufuzu hatua ya robo fainali, akisisitiza umuhimu wa kutumia kila fursa wanayopata mbele ya mashabiki wao katika Uwanja wa Emirates.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika mchezo wa kwanza, Arsenal walinusurika kupoteza baada ya mshambuliaji Kai Havertz kufunga penalti dakika ya 89 dhidi ya klabu yake ya zamani, bao lililowapa matumaini ya kusonga mbele.
Kocha huyo alieleza kuwa ameifuatilia Leverkusen walipocheza dhidi ya Bayern Munich na kubaini kuwa ni timu iliyopangwa vizuri, yenye mbinu thabiti na inayofundishwa kwa kiwango cha juu.
Hata hivyo, Arsenal watamkosa nahodha wao Martin Odegaard pamoja na beki Jurrien Timber kutokana na majeraha, huku mshambuliaji Leandro Trossard akithibitishwa kuwa fiti kurejea uwanjani. Aidha, beki Ben White ameanza mazoezi na yuko tayari kusaidia timu.
Kwa ujumla, Arteta anaamini kuwa pamoja na changamoto zilizopo, Arsenal wana nafasi kubwa ya kufuzu iwapo watazingatia mpango wa mchezo, kutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani na kupambana kwa nidhamu dhidi ya wapinzani wao waliopangika vizuri.

