Bongo Zozo atia timu kwenye mazoezi ya Taifa Stars; Ampa tuzo ya heshima kocha Kim Paulsen; mchezaji noma wa Bongo zozo kupata tuzo na pesa taslim.

Mhamasishaji na shabiki kindakindaki wa timu ya taifa ya Tanzania, Bongo Zozo ametembelea kambi ya taifa stars na kutoa tuzo ya kinywaji cha bia ambacho ni sehemu ya wadhamini wa timu ya  hiyo.

Bongo Zozo Atoa Tuzo ya Bia kwa kocha Kim.

Mbali na hayo pia amesema kuwa ametengeneza tuzo maalum kwa mchezaji atakayecheza vizuri kwenye mechi dhidi ya Uganda tarehe 28 Agosti, ameongeza kuwa tuzo hiyo itaambatana na kiasi kidogo cha pesa.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by mkazuzutza (@mkazuzutza)

“Kuna tuzo ya mchezaji noma imetengenezwa na mimi, mchezaji noma wa bongo zozo nitampa hii tuzo na hela kidogo, sio hela mamilioni lakini sio buku jero pia”

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa