Simba Queens timu ya wanawake ya Simba inayoshiriki kombe la mabingwa Afrika mashariki ya Cecafa dhidi ya She Corporates ya nchini Uganda.

Simba ambayo imefanikiwa kufika fainali ya michuano  hiyo baada ya kuifunga As Kigali ya Rwanda kwa jumla ya magoli matano kwa moja kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa katika dimba la Azam complex Chamazi jijini Dar-es-salaam.

simba queens, Simba Queens Kucheza Fainali Cecafa Leo., Meridianbet

Pia Simba Queens ilicheza michezo mitatu kwenye hatua ya makundi nas kushinda michezo yote mitatu kabla ya kuvaana na klabu ya As Kigali kwenye hatua ya nusu fainali.

Kwenye mchezo wa fainali leo ambapo klabu ya Simba Queens watacheza na She Corporates ya Uganda timu hizi zilikutana kwenye makundi na Simba Queens kushinda mabao mawili kwa bila kitu kinachofanya mechi hii kua na mvuto zaidi wapennzi wa soka wakisubiri kama She Corporates watalipiza kisasi au Simba Queens wataendeleza ubabe.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa