Manchester United yaendelea ilipoishia kwenye mchezo ulioisha dhidi ya Liverpool mwanzoni mwa wiki hii.

Mapema leo katika majira ya saa nane na nusu mchana Man united ilikua uwanjani katika dimba la St. Marrys Park wakikaribishwa na wenyeji wao Southampton wakifanikiwa kushinda kwa bao moja kwa billa goli pekee lililofungwa kwenye mchezo huo liliwekwa kimiani na kiungo wa kireno Bruno Fernandes dakika ya 55 ya mchezo.

man united, Man United Yatakata ugenini., Meridianbet

Hii inawafanya Man United kua na alama sita kwenye michezo minne waliocheza kwenye ligi kuu ya Uingereza.

United wanapata ushindi wa pili mfulululizo baada ya kuanza vibaya ligi hiyo kwa kupoteza michezo miwili ya awali lakini leo wameendelea kutakata kwa kupata ushindi mwingine katika kiwanja cha ugenini.

Kwa upande mwingine nahodha wa ttimu hiyo Harry Maguire ameendelea kusugua benchi huku Raphael Varane pamoja na usajili mpya beki wa kiajentina Lisandro Martinez wakitengeneza pacha kwenye ukuta wa timu hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa