Wakati wakitarajia kucheza mechi ya kirafiki leo dhidi ya Taifa Jang’ombe kikosi cha Azam FC pia kitajipima dhidi ya As Arta Solar 7 ya nchini Djibout.

Azam FC tayari wapo Zanzibar kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar saa 2:15 usiku wa leo.

Akizungumzia hilo Ofisa Habari wa Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amesema kuwa “Kikosi kipo Zanzibar tayari kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Taifa Jang’ombe ambao wametualika kwenye tamasha lao.

Azam FC
Azam FC

“Baada ya mchezo huo timu itarejea Dar kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya As Arta Solar 7 ya nchini Djibout mechi hiyo tutacheza Agosti 31 kwenye Uwanja wa Azam Complex.

“Michezo hiyo miwili ya kirafiki katika kipindi hiki cha mapumziko kitampa kocha picha halisi ya kikosi chake baada ya kufanya marekebisho kufuatia michezo miwili ya ligi tuliyocheza awali.”


Kwa taarifa za kimichezo na uchambuzi sasa unaweza kutazama video hizo kwa kupitia youtube . USISAHAU KU SUBSCRIBE

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa