KAMA ulidhani Singida Big Stars wamemaliza usajili basi sio sahihi kwani taarifa ni kwamba wamemshusha nyota mpya raia wa Argentina, Miguel Escobar.

Nyota huyo ametambulishwa na Singida Big Stars akicheza nafasi ya kiungo mshambuliaji ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na kocha Mkuu, Hans van der Pluijm.

Singida Big Stars
Singida 

Escobar tayari amejiunga na kikosi hicho ambacho kimeweka kambi Mkoani Mwanza kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya ligi ambayo inatarajia kuanza Septemba 6 mwaka huu.

Kikosi cha Singida Big Stars kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba Agosti 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Singida katika michezo miwili ya ligi waliyocheza wamefanikiwa kuvuna pointi zote sita dhidi ya Tanzania Prisons (1-0) na Mbeya City (2-1).


Kwa taarifa za kimichezo na uchambuzi sasa unaweza kutazama video hizo kwa kupitia youtube . USISAHAU KU SUBSCRIBE

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa