BAADA ya kualikwa kwenye mashindano na Al Hilal ya Sudan, Bosi wa amatajiri wa kariakoo mitaa ya msimbazi amefunguka kuwa mipango yao ya kushiriki mashindano hayo ni kutwaa ubingwa.

Simba wananatarajia kushuka dimbani kesho jumapili kumenyana na Asante Kotoko ya Ghana ambayo pia imealikwa katika mashindano hayo.

Akizungumza baada ya kuwasili nchini Sudan, Mratibu wa timu hiyo, Abbas Ally amesema kuwa “Tumefika salama baada ya safari ya muda mrefu na leo kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho.

Simba

“Sisi tulivyo andaa yake mashindano ya Super Cup tuliibuka kuwa mabingwa lakini watu waliongea sana kwamba tumejiandalia wenyewe, sasa hivi tumealikwa tunataka kuwa mabingwa wa haya mashindano.”

 


Kwa taarifa za kimichezo na uchambuzi sasa unaweza kutazama video hizo kwa kupitia youtube . USISAHAU KU SUBSCRIBE

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa