Simba queens timu ya wanawake ya Simba imefanikiwa kushinda ubingwa wa kombe Afrika mashariki unaojulikana Cecafa.

Simba queens walifanikiwa kuifunga klabu ya She Corporates ya nchini Uganda bao moja kwa bila lililofungwa na Aquino Corazone dakika ya 47 ya mchezo.

simba queens, Simba Queens Mabingwa Cecafa., Meridianbet

Simba wanafanikiwa kua timu ya kwanza kua timu ya kwanza kua bingwa wa michuano hii pia michuano hii ilikua inatumika kutafuta muwakilishi wa Afrika mashariki kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika upande wa wanawake.

Simba queens wanafanikiwa kubeba taji hilo kwa rekodi ya aina yake baada ya kucheza michezo mitano na kushinda michezo yote mitano na kufunga mabao kumi na nane na kuruhusu bao moja tu.

Pia Simba queens walitawala kwenye tuzo za michuano hiyo kwani walitoa tuzo ya mchezaji bora wa michuano Aquino Corazone,pamoja na golikipa bora mashindano Gelwa Yona kutokea Simba queens.

Ni rasmi Simba queens wanakwenda kua wawakilishi pekee wa ukanda huu wa Afrika mashariki kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa