Chelsea Kupiga Kura Anthony Taylor Kutocheza Michezo Yao

Mashabiki zaidi ya n 100,000 walitia saini kwenye mtandao wa change.org ili kutaka mwamuzi aliyechezesha mchezo wa jumamosi Anthony Taylor kufungiwa kuchezesha michezo ya chelsea kutoka na kilichotoeka kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya 2-2.

Ombi hilo limetokana na maamuzi 12 yaliofanywa na Taylor kwenye miaka ambayo yanakusudi ya kuthibitisha kuwa mwamuzi ana ajenda dhidi ya klabu ya Chelsea, wakati YouTube walikusanya vipande vya hizo video ambazo zilitizamwa na mara 140,000 siku ya Jumatatu na kulikuwa na ongezeko la zaidi ya watu elfu kumi kwa kila saa.

Thomas Tuchel kwenye mchezo huo alimshtumu kocha huyo baada ya mchezo kuisha na kudai kuwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo walikuwa wanamjadili, lakini baada ya mchezo kuiasha alipokutana na waandishi wa habari hakucha kumtolea lawama yeye na waamuzi waliokuwa kwenye VAR.

Thomas Tuchel alipoulizwa kuhusu ikiwa ni bora kama Taylor asiwe mwamuzi wa michezo ya Chelsea tena, Tuchel alijibu: “Huenda itakuwa bora. Lakini kiukweli, Tulikuwa na VAR ya kutusaidia kufanya maamuzi  sahihi. Tang lini chezaji akavutwa nywle? Tangu lini hilo?  Na kama hakuona siwezi hilo, siwezi kumlaumu.

“Sikuona hilo, lakini kuna watu kwenye VAR ambao wanaangalia hili na kisha kukuonyesha na kwanini hii haiwezi kuwa  free-kick na kwanini hii haikuweze kuwa Kadi nyekundu? Inakuwaje?”

 

 

Acha ujumbe