Mara baada ya Ronaldo kuwajibu wale wanaomhusisha kuondoka hatimaye sasa huenda ikawa hivyo, kabla ya dirisha kubwa kufungwa mwezi Septemba ambapo anahusishwa Zaidi na Atletico Madrid inayoshiriki ligi ya mabingwa wa Ulaya UCL.

Mshahara wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 37 ni kikwazo kikubwa, na ripoti zinaonyesha kuwa sasa ana ushawishi mbaya huko Manchester United, baada ya klabu hiyo kuanza vibaya msimu huu kwa kupoteza mechi zote mbili walizocheza kwa kufungwa jumla ya mabao 6.

Meneja Erik ten Hag amesema Ronaldo hauzwi, lakini msimamo huo ulibadilika siku ya Jumanne na hatimaye klabu ipo tayari kumwachia, na wakala wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno Jorge Mendes atakuwa na nia ya kutaka kuhamia Atletico Madrid.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa