Kwa muda mrefu kumekuwa na taarifa nyingi sana kumhusu mshambuliaji muandamizi wa Manchester United Christian Ronaldo, kuwa ataondoka katika viunga vya Old Trafford Jijini Manchester huku akihusishwa Zaidi na timu nyingi.

Timu anazohusishwa nazo, ni pamoja na mahasimu wa UTD Watoto wa Pep Guadiola Manchester City, kwa upande mwingine amekuwa akiandikwa kwenye vichwa vingi vya habari kuwa ataondoka Manchester na kujiunga Chelsea.
Baada ya Staa huyo kukaa kimya kwa muda mrefu bila kujibu chochote hatimaye ameamua kuvunja ukimya na kuandika Taarifa kuhusu uvumi huo na kuelezea hatma yake katika klabu yake ya sasa ambayo tayari amerejea uwanjani tena, Ronaldo ameandika kuwa
“Nyote mtaujua ukweli wote pale nitakapofanya Mahojiano hivi karibuni, vyombo vya habari vimekuwa vikisambaza uongo na katika kitabu change kati ya habari 100 zilizoandikwa kunihusu mimi ni 5 tu kati ya hizo zina ukweli mnaweza kuona jinsi ilivyo, zingatieni hizo Takwimu”
– Amesema Ronaldo.
Mashabiki zake wameonesha kufurahia kauli hii na wengi kati yao wamemsifia Staa huyo Raia wa Ureno kwa kuviambia ukweli vyombo vingi vya habari vinavyotumia ukubwa wa jina la Ronaldo kujipatia wafuasi wengi kwenye mitandao yao ya kijamii.

