Klabu za Manchester United na Chelsea zimeonesha nia ya kumtaka Kiungo wa Barcelona, De Jong baada ya kile kinachosemekana klabu yake ya sasa inakumbukwa na kikwazo cha sheria ya mshahara kwenye ligi ya LaLiga nchini Hispania.

Kiungo huyo wa kati wa Uholanzi hajawahi kusema wazi kwamba anataka kuondoka Nou Camp, ila amekuwa akizungumza zaidi kuhusu nia yake ya kubaki, lakini matatizo ya kifedha ya upande wa La Liga yanamaanisha kuwa wanaweza kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ili kusaidia kusawazisha vitabu.

De jong, De Jong Kuhusishwa na Manchester United na Chelsea, Meridianbet

 

Suala la kimkataba kuhusu mishahara iliyoahirishwa ndio sababu kuu iliyoripotiwa kusitishwa kwa dili hilo, na sasa Chelsea wanaotumia pesa nyingi wanaelekea kuwapiku Manchester United ambao nao mapema tu walionesha nia ya kumtaka kiungo huyo.

Awali mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi alishakataa kujiunga na klabu ya Manchester United licha ya klabu ya Barcelona kukubali offer ya klabu hiyo iliyo na makazi yake pembezoni mwa jiji la Manchester.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa