Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amezidi kusisitiza kuwa kiungo raia wa Uholanzi Frenkie de Jong hauzwi kwenda klabu yoyote msimu huu licha ya kuwa, kuna makubaliano waliyashayafanya na klabu ya Manchester United.

Wiki iliyoisha klabu ya Barcelona walikubali kumuuza De Jong kwenda klabu ya Manchester United  kwa kiasi cha £ 65milion, kabla ya rais huyo kutoka hadharani kupinga kuwa hayuko tayari kumuachia kiungo huyo.

Frenkie de Jong

De Jong alisajiriwa na klabu ya Barcelona mwaka 2019 kwa ada ya uhamisho ya kiasi £65milion, ikiwa Barcelona wangefanikiwa kuchukua ubingwa basi waneongeza kiasi cha £9.5milion kwenye ada ya uhamisho huo.

Joan Laporta anaamini kuwa anaweza kumbakisha Frenkie de Jong, kwa sababu moja ya wachezaji waliokubali kupungumza mshahra wake naye ni mmoja wapo.

Ikiwa uhamisho wa Frenkie de Jong utakamilika basi atakuwa anaungana na kocha wake wa zamani kwenye klabu ya Ajax.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa