Guardiola: Sitafundisha Klabu Nyingine Baada ya Man City

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ameweka wazi hana mpango wa kufundisha klabu nyingine yeyote baada ya kumaliza mkataba wa ndani ya klabu hiyo mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza.

Guardiola hajioni kama akiondoka ndani ya klabu ya Manchester City atakwenda kufundisha klabu nyingine yeyote nchi nyingine kwa upande wa klabu anaona kama atakua amemaliza, Kocha huyo ameweka wazi labda timu ya taifa ambapo pia hajaweka kama kuna uwezekano mkubwa kutumkia upande huo.Guardiola

“Sitaenda kusimamia klabu nyingine yoyote baada ya City.”

“Sisemi kuhusu maisha ya baadaye ya muda mrefu, lakini ninachosema ni kwamba sitafanya hivi: kuondoka, kwenda nchi nyingine, kufanya kile kile ninachofanya sasa.”

“Labda timu ya taifa, lakini hiyo ni tofauti.”

Kuna kila dalilia inayoonesha kua kocha Guardiola hana muda mrefu kufundisha soka haswa upande wa vilabu na ndio sababu akisema labda upande wa timu ya taifa inaweza kua ndio kimbilio lake, Hata hivyo kocha huyo raia wa kimataifa wa Hispania ameshafanya makubwa kwenye ulimwengu wa soka hivo hata akiamua kupumzika atakua hana deni.

Acha ujumbe