Yanga na Mazembe Ni Vita leo Lubumbashi

Mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya klabu ya Yanga dhidi ya Tp Mazembe unaotarajiwa kupigwa mida ya saa 10 jioni ni mchezo ambao una picha ya aina yake kwani vilabu vyote viwili vinahitaji kupata matokeo kwenye mchezo huu.

Yanga watakua ugenini kwenye mchezo huu ambao unatarajiwa kupigwa nchini DR Congo katika jiji la Lubumbashi ambapo mchezo wa leo utakua na ushindani mkubwa sana kwani mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Tanzania wamepoteza mechi zao mbili za awali kwenye ligi ya mabingwa Afrika mpaka sasa na wanaona mchezo wa leo kama nafasi ya kuweza kufufuka.yanga

Tp Mazembe ambao ni wenyeji wa mchezo wa leo nao hawako kwenye mazingira mazuri kwani wameshapoteza mchezo mmoja na kusuluhu mmoja katika michezo yao miwili waliyocheza, Hivo nafasi yao ya kuweza kupata matumaini ya ksonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ni kuhakikisha wanashinda mchezo wa leo wakiwa nyumbani.

Kila timu leo itahitaji kupata matokeo ya ushindi ili kufufua matumaini ya kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali hivo sio kwa Yanga wala Tp Mazembe ambaye atauchukulia mchezo huu kiuwepesi, Na hili ndio jambo ambalo linafanya mchezo huu uwe na mvuto mkubwa sana na kua wenye ushindani pia.

Acha ujumbe