Jana katika Mchezo wa Ligi ya Mabingwa UEFA Historia mbalimbali ziliandikwa katika fainali hiyo. Zifuatazo ni Historia mbalimbali zilizoandikwa jana:

Thomas Tuchel Fainali yake ya pili anabeba Kombe la UEFA kwa Mara ya kwanza. Gurdiola kwake UEFA  anaikosa na anakuwa aanandika rekodi ya kufika fainali 16 na fainali 2 tu kukosa Kombe.

 

Kwa timu ya kwanza kuingia Fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza haijawahi kuchukua Kombe hili la UEFA Champions League, Manchester City wameingia katika rekodi hiyo hapo jana.

Chelsea inakuwa timu ya 3 England kutwaa UEFA zaidi ya mara moja wakiongozwa na Liverpool mwenye makombe 6 akifatiwa Manchester United mwenye makombe 3.

Thiago Silva kwa Mara ya kwanza anatwaa Ligi ya Mabingwa hii baada ya kucheza Fainali ya kombe hilo mara mbili mfululizo moja akiwa PSG moja akiwa Chelsea.

Ng’olo Kante anacheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa UEFA kwa mara ya kwanza na kutwaa ubingwa, Tangu ajiunge na Leicester mwaka 2013 mpaka mwaka 2021 ni mwaka 2020 ambao hajatwaa taji miaka mingine yote amenyanyua ndoo katika ngazi ya klabu na timu ya taifa.

Manchester city anamaliza msimu huu akiwa mkononi na makombe 2, Ligi na Carabao Cup, Ila anakosa UEFA bado anaandika historia yake ya kucheza Fainali kwa mara ya kwanza kabisa.

 

Hii inakuwa Fainali ya pili kwa timu za England kukutana kwa pamoja, Fainali ya kwanza ni mwaka 2019 kati ya Liverpool dhidi ya Tottenham.

Foden anakuwa mchezaji mwenye umri mdogo katika Klabu ya Manchester City kucheza fainali hii kwa mara ya kwanza.

Mendy anakuwa golikipa wa kwanza wa Afrika kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa na kutwaa Kombe hilo.

Uwanja wa estadio De lapot wa klabu ya FC Porto unakuwa uwanja wa kwanza kuchezewa Fainali 3 za Ligi ya Mabingwa UEFA.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa