Luis Díaz Njiapanda, Hatma Yake Haieleweki

Nyota wa klabu ya Liverpool, Luis Diaz, anazidi kuhusishwa na vilabu vya Barcelona na Bayern Munich, huku mustakabali wake ukiwa kitendawili kinachovuta macho ya mashabiki wa soka barani Ulaya.

 

Luis Díaz Njiapanda, Hatma Yake Haieleweki

Kwa sasa, Barcelona wanaendelea kuwa na matumaini ya kupata saini ya mchezaji huyo, lakini wanakumbwa na changamoto za kifedha na masuala ya usajili. Klabu hiyo inahitaji kuhakikisha Díaz anasajiliwa rasmi kabla ya tarehe 31 Agosti, vinginevyo mkataba utahitaji kipengele cha fidia (compensation clause) jambo ambalo linaweza kuwa kikwazo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Luis Díaz Njiapanda, Hatma Yake Haieleweki

Wakati huo huo, Bayern Munich wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri zaidi. Klabu hiyo ya Ujerumani ipo tayari kutuma ofa ya €60 milioni pamoja na nyongeza ya hadi €20 milioni kama bonasi, ofa ambayo inaweza kufikia mahitaji ya Liverpool.

Kwa upande wa Liverpool, msimamo ni kwamba Díaz si mchezaji wa kuuzwa, isipokuwa wakipokea ofa inayokaribia €80 milioni au zaidi. Klabu hiyo bado inamthamini sana mshambuliaji huyo ambaye ana mkataba hadi mwaka 2027, lakini ikiwa hawatamwongezea mkataba mpya, wanaweza kulazimika kufikiria kumuuza sasa.

Luis Díaz Njiapanda, Hatma Yake Haieleweki

Díaz mwenyewe bado hajafanya maamuzi ya mwisho, lakini amethibitisha kuwa anapendezwa na mipango ya vilabu vyote viwili na atasikiliza kile ambacho “kitakuwa bora kwa maisha yake ya baadaye.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.