Romelu Lukaku anaripotiwa kuwa tayari anatazamia kuongeza muda wake wa kusalia katika klabu ya Inter Milan zaidi ya msimu huu kufuatia kurejea kwake Chelsea.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alirejea San Siro kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Chelsea msimu huu wa joto, na kwa mujibu wa La Gazzetta dello Sport, mshambuliaji huyo hana mpango wa haraka wa kurejea Stamford Bridge.

 

lukaku

Maafisa katika klabu hiyo ya Serie A wanaaminika kupanga kubadilisha mkataba wake wa mkopo ili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 aongeze muda wa kusalia Milan hadi mwisho wa msimu wa 2023-24.

Inter walimnyakua Lukaku mnamo 2019 baada ya kipindi kigumu huko Manchester United. Mbelgiji huyo alianzisha ushirikiano wa hali ya juu na mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez na wawili hao wakaisaidia Inter kutwaa taji lao la Serie A mnamo 2021 ikiwa ni baada ya kukaa miaka 11 bila taji hilo.

 

lukaku

Uhamisho wa Lukaku kwa paundi milioni 100 kwenda Chelsea mwaka 2021 haukuwa na mpango baada ya kushindwa kuonesha kiwango chake alichokionyesha kwenye Serie A na baadaye akafukuzwa benchi na kocha wa zamani Thomas Tuchel.

 

lukaku

Wakati huo huo, beki wa Inter Alessandro Bastoni ameonekana kuwavutia Manchester United na Manchester City huku bosi wa zamani wa Inter Antonio Conte pia akimfuatilia mchezaji huyo mwenye miaka 23 ili kuhamia Tottenham.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa