Lionel Messi alizomewa na mashabiki wa Paris Saint-Germain katika mchezo wake wa kuiaga klabu hiyo. Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.
Kabla ya mechi yao ya mwisho ya msimu huu, kocha wa PSG Christophe Galtier alifichua kwamba Messi ataondoka msimu huu wa joto.
Messi alicheza kwa mara ya mwisho na mabingwa hao wa Ligue 1 katika pambano lao la nyumbani dhidi ya Clermont Jumamosi usiku, ambalo liliisha kwa kushindwa 3-2.
Alizomewa wakati wa mechi na kisha tena wakati wa kukabidhiwa kombe wakati jina lake likitajwa. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Kabla ya mechi hiyo kuanza, PSG ilithibitisha kuwa mshindi huyo mara saba wa tuzo ya Ballon d’Or ataondoka kabla ya msimu ujao.
Walisema: “Baada ya misimu miwili katika mji mkuu wa Ufaransa, safari ya Leo Messi na Paris Saint-Germain itakamilika mwishoni mwa kampeni ya 2022-23.
“Klabu ingependa kutoa shukrani zake za dhati kwa mshindi huyo mara saba wa Ballon d’Or, ambaye pia alinyakua Trophée des Champions na mataji mawili ya Ligue 1 akiwa na Les Rouge et Bleu.”
Imeripotiwa kuwa huenda akatimkia Saudi Arabia, huku Al Hilal akitaka kuwa klabu ya tatu katika maisha yake ya soka. Ukiwa na meridianbet unapata odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.
Kabla ya kuondoka kwake Messi aliiaga PSG, klabu ambayo imeendelea kushinda mataji katika maisha yake ya soka. Pata odds kubwa kutoka Meridianbet kwa mechi za ligi mbalimbali.
Alisema: “Ningependa kuishukuru klabu, jiji la Paris na watu wake kwa miaka hii miwili. Nawatakia kila la kheri kwa siku zijazo.”