Onyango hafurahii kukaa benchi.

Beki kimataifa wa Simba SC raia wa kenya Joash Onyango ambaye alifanya vizuri kwenye misimu miwili ya Ligi kuu akiwa na wakongwe hao kwenye mpira wa miguu hapa tanzania, ambapo tangu msimu huu wa ligi kuu 2022/2023 kuanza Onyango amekuwa akiishia kukaa benchi tu.

Msimu uliopita Onyango alikuwa akicheza sambamba na Henock Inonga au Pascal Wawa ambaye kwa sasa hayupo kikosini hapo, lakini mara baada ya usajili wa baadhi ya wachezaji hususani kwenye eneo la ulinzi, Simba wamemsajili beki wa kati kutoka Al Hilal ya nchini Sudan ambaye amekuja kuchukua nafasi iliyoachwa na Wawa. Beki huyo ameonekana kumkosha kocha wa klabu ya Simba Zoran Maki kwa kumpanga katika kikosi chake cha kwanza huku Onyango akianzia benchi.

Msemaji wa klabu hiyo Ahmed Ally amezungumzia kitendo hicho cha Onyango kukaa benchi kuwa kinamkosesha raha ambapo alisema “inawezekana ni kweli Onyango hana raha”

Inawezekana kwa sababu amepoteza nafasi yake ya kucheza, Joash ilikuwa ni panga pangua msimu uliopita yeye na Inonga, msimu huu amekuwa hana nafasi, mechi mbili za ligi kuu hajapatra nafasi ya kuanza, hii lazima itamtoa mchezoni hakuna mtu anayependa kukaa benchi haswa kwa mchezaji kama Joash ni mchezaji mkubwa kweli kweli

Ahmed aliyasema hayo alipoulizwa na wasafi fm kuhusiana na hali ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Kenya.

Acha ujumbe