Real Madrid wanahusishwa na uhamisho wa staa wa Everton Richarlison, kwa mujibu wa ripoti kadhaa.

Staa huyu wa miaka 25 amesalia na miaka miwili kwenye mkataba wake wa sasa na klabu yake, na Real Madrid tayari wamemuweka nyota huyu kwenye rada zake.

Real Madrid hawapo peke yake kwenye windo la staa huyu wakifuatana na klabu za Tottenham Hotspur na Paris Saint-Germain.

Richarlison amefanikiwa kucheka na nyavu mara sita kwenye gemu tisa za mwisho za EPL akiwasaidia Everton kuepuka kikombe cha kushuka daraja.

Richarlison, aliingia Ulaya msimu wa joto wa 2017 alipoungana na Watford kutoka Fluminense, aliondoka na kwenda Goodson Park mwaka mmoja baadaye.

Staa huyu amechangia jumla ya magoli 43, na asisti 14 kwenye michezo 152 akiwa na Everton.

Real Madrid hawapo peke yao katika kuifukuzia saini ya staa huyu, lakini huenda akafanikiwa kuleta ushindani mkubwa zaidi katika vilabu vinavyohitaji huduma yake.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa