Mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo alirejea uwanjani kwa kishindo baada ya kuukosa mwezi mmoja kutokana na majeraha, akifunga mabao mawili na kusaidia Al Nassr kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Al Najma katika Ligi Kuu ya Saudi.
Ronaldo, ambaye alikuwa nje tangu Februari, alikosa michezo miwili ya ligi pamoja na mechi za kirafiki za timu ya taifa ya Ureno dhidi ya Mexico na Marekani, lakini alionyesha kiwango cha juu mara baada ya kurejea kikosini.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika mchezo huo, Al Najma walishangaza kwa kufungua bao dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Rakan Al Tulayhi, kabla ya Al Nassr kusawazisha na kisha kuongoza kupitia mabao ya Abdullah Al Hamdan na Sadio Mane katika muda wa nyongeza wa kipindi cha kwanza.
Al Najma walirejea mchezoni mapema kipindi cha pili kupitia bao la Felippe Cardoso, lakini Ronaldo alirejesha uongozi kwa mkwaju wa penalti dakika ya 56, akionyesha utulivu mkubwa mbele ya lango.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 aliongeza bao la pili dakika ya 73, kabla ya Mane kufunga bao la mwisho dakika za nyongeza na kuhitimisha ushindi huo mnono kwa Al Nassr.
Ushindi huo ulikuwa wa 13 mfululizo kwa Al Nassr kwenye ligi, ukiwaweka kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 70, sita zaidi ya wapinzani wao wa karibu Al Hilal, ambao wanatarajiwa kucheza dhidi ya Al Taawoun.

